Machapisho

Picha
Mamoudou Gassama: 'Spiderman' aliyeishangaza Ufaransa kwa kumuokoa mtoto kutoka kwenye jengo la ghorofa apewa uraia Mhamiaji wa Mali amepongezwa kama shujaa baada ya kukwea sehemu ya mbele ya jengo la ghorofa mjini Paris kumuokoa mtoto aliekuwa kwenye uzio wa ubaraza wa ghorofa ya nne kwenye jengo refu. Video ya Mamoudou Gassam akimuokoa mtoto ilisambaa sana kwenye mitandao ya kijamii. Alivuka kutoka kwenye ubaraza mmoja hadi mwingine kwa muda wa chini ya dakika moja akamvuta mtoto huyo aliyekuwa amekwama na kumsalimisha Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron baadaya kukutana na Bw Gassama kwenye makazi yake ya Elysee Palace Jumatatu kumshkuru binafsi alitangaza kumpa uraia wa taifa hilo.

JE? REAL MADRID WATAMSAJILI SALAH

Picha
mo salah hatakuwa tayari kujiunga na mabingwa wa ulaya kutokakana kitendo kilichofanywa na beki kisiki na kapteni wa real madrid..........kuwa si kitendo cha kiungwana ..............ameyasema hayo baada ya kuhojiwa na kituo kimoja mjin kiyv

ALIYONENA ZIDANE BAADA YA KUTWAA UBINGWA

Picha
HAYA NDIYO MANENO YA ZIDANE Zinedine Zidane amesema anajivunia kuweka historia na Real Madrid baada ya kunyakua taji la ligi ya mabingwa dhidi ya Liverpool siku ya Jumamosi. Real Madrid ilishinda mabao 3-1 huku Gareth Bale akifunga magoli mawili Real ni timu yenye mafanikio zaidi kwenye historia ya ligi ya mabingwa ikiwa na mataji 13. Zidane alisema:''hii ni klabu ya wakongwe. Klabu hii imeshinda makombe 13 ya Ulaya nafurahi kuwa sehemu ya historia hii Aliongeza: '' tunakwenda kufikiria kuhusu tulichokipata, kufurahia wakati huu kwanza.Ni kitu muhimu zaidi kwa sasa''.
Picha
real madrid yatwaa ubingwa wa ulaya
Picha
Akizungumza jijini Dar es salaam Afisa habari wa Azam FC Jaffary Iddy Maganga amesema, mjadala wa kuondoka kwa Farid ulikuwa ni mrefu lakini wanashukuru kila kitu kimefanikiwa na wanaamini atacheza kwa mafanikio ili kufungua milango kwa wachezaji wengine wa Tanzania kuweza kufika mbali zaidi katika soka. Kwa upande wake Farid amesema, amejiandaa vizuri kwa ajili ya kwenda kucheza na siyo kwa ajili ya majaribio kama ilivyokuwa hapo awali na amejiandaa kukabiliana na changmoto atakazokutana nazo lakini kubwa zaidi amejipanga kupambana kwa ajili yake pamoja na taifa kwa ujumla
Picha
Wenger: Ozil atawashangaza wakosoaji wake Mkufunzi wa Arsenal Arsene Wenger anasema kuwa kiungo wa kati wa Arsenal Mesut Ozil atawashangaza wakosoaji wake katika mechi inayofuata. Ozil alikosolewa vibaya baada ya Arsenal kushindwa 2-1 na Manchester City . Lakini Wenger amesema kuwa Ozil kama wachezaji wengine shupavu katika timu yake amekuwa akichukua jukumu kubwa na hivyobasi hapaswi kulaumiwa sana. Anasema kwamba tatizo la Arsenal kupoteza mechi hiyo ilikuwa kushindwa kudhibiti mchezo katikatika ya uwanja. Wenger: Wachezaji kama Ozil wanapokosolewa wao hujibu kwa kucheza vizuri katika uwanja katika mechi inayofuata.
Picha
JE. USIKIA ALICHOKISEMA PEP GUARDIOLA Mkufunzi wa klabu ya Manchester City Pep Guardiola anasema kuwa itakuwa vigumu kwa kikosi chake kushindana na viongozi wa ligi ya Uingereza Chelsea. City ilipanda hadi nafasi ya pili katika jedwali baada ya kuicharaza Hull City 3-0 katika siku kuu ya Boxing Dei na kuweza kuwa nyuma ya Chelsea kwa pointi 7. Kikosi hicho cha Antonio Conte awali kiliweka rekodi ya kushinda mara 12 katika ligi ya Uingereza baada ya kuichapa Bournemouth 3-0. ''Tumecheza mechi saba zaidi ya Chelsea ,ndio maana ni vigumu '',alisema Guradiola. ''Liverpool ilikaribia taji hilo mwaka mmoja uliopita kwa sababu walikuwa na mechi moja kwa wiki ,na ni hivyo ndivyo ilivyokuwa na Leicester.Mara hii Chelsea na Liverpool wana fursa''. Liverpool na Chelsea zilishindwa kufuzu katika mashindano ya Ulaya baada ya kumaliza wa nane na 10 mtawalia katika ligi ya Uingereza mwaka uliopita. shebyperfect.blogspot.com