
Akizungumza jijini Dar es salaam Afisa habari wa Azam FC Jaffary Iddy Maganga amesema, mjadala wa kuondoka kwa Farid ulikuwa ni mrefu lakini wanashukuru kila kitu kimefanikiwa na wanaamini atacheza kwa mafanikio ili kufungua milango kwa wachezaji wengine wa Tanzania kuweza kufika mbali zaidi katika soka. Kwa upande wake Farid amesema, amejiandaa vizuri kwa ajili ya kwenda kucheza na siyo kwa ajili ya majaribio kama ilivyokuwa hapo awali na amejiandaa kukabiliana na changmoto atakazokutana nazo lakini kubwa zaidi amejipanga kupambana kwa ajili yake pamoja na taifa kwa ujumla