
Mamoudou Gassama: 'Spiderman' aliyeishangaza Ufaransa kwa kumuokoa mtoto kutoka kwenye jengo la ghorofa apewa uraia Mhamiaji wa Mali amepongezwa kama shujaa baada ya kukwea sehemu ya mbele ya jengo la ghorofa mjini Paris kumuokoa mtoto aliekuwa kwenye uzio wa ubaraza wa ghorofa ya nne kwenye jengo refu. Video ya Mamoudou Gassam akimuokoa mtoto ilisambaa sana kwenye mitandao ya kijamii. Alivuka kutoka kwenye ubaraza mmoja hadi mwingine kwa muda wa chini ya dakika moja akamvuta mtoto huyo aliyekuwa amekwama na kumsalimisha Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron baadaya kukutana na Bw Gassama kwenye makazi yake ya Elysee Palace Jumatatu kumshkuru binafsi alitangaza kumpa uraia wa taifa hilo.